Wenger: “ Siwezi kurudi kufanya kazi England “
Arsene Wenger amefufua upya habari ya yeye kurudi katika soka mapema mwanzoni mwa mwaka ujao ila sasa amesema haitokuwa nchini England.
Akihojiwa na kituo cha Sky Sports katika wa Wembley Mfaransa huyu aliyeshinda mataji mengi ya FA (7) kuliko meneja mwingine yeyote kwenye historia na hata kuliko baadhi ya timu kubwa alisema “Nipo hapa Wembley nilipocheza michezo mingi, na nikiwa na kumbukumbu nyingi nzuri sana .
Nimeshasema mara nyingi kuwa nimetumia muda mwingi hapa England tena katika klabu moja, hivyo itakuwa ni vizuri nikienda sehemu nyingine sasa.
Siwezi sema ni wapi kwa sasa sababu mimi mwenyewe binafsi bado sijajua na wala sijaamua.”
Mfaransa huyo amekuwa akihusishwa na klabu ya Real Madrid hasa baada ya kocha Julen Lopetegui kutimuliwa na pia amehusishwa kutakwa na klabu ya PSG kama mkurugezi wa ufundi katika klabu hiyo.