“TUMEKUJA NA JESHI LETU KAMILI KUWAKABILI LIPULI FC” CANNAVARO
Baada ya kuwasili salama mkoani Iringa, Kikosi cha Yanga SC kimefanya mazoezi yake ya mwisho katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wake dhidi ya Lipuli FC.
Meneja wa Klabu hiyo Haroub Cannavaro amesema kuwa wameenda mkoani Iringa na jeshi kamili kwaajili ya kuwakabiri Lipuli hapo kesho.
” Tunamshukuru Mungu tulifika salama hapa Iringa na tumekuja na jeshi kamili kwa ajili ya kuwakabili Lipuli na tunaamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa kesho tutakaocheza hapa Iringa, cha msingi wapenzi na mashabiki wetu waendelee kutuombea tufanye vizuri”amesema Cannavaro.

Yanga anakutana na Lipuli akiwa amecheza mechi 27 na anashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi na point 67, Lipuli FC amecheza michezo 30 anashika nafasi ya sita na point 41