Azam na Singida waipa heshima Simba
Mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara kati ya Azam FC na Singida United uliopangwa kuchezwa machi 16 (jumamosi) katika Uwanja wa Azam Complex sasa kuchezwa kesho Ijumaa Machi 15.
Jaffar Iddi Maganga ambae ni Afisa habari wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa kutokana na Bodi ya ligi kuwapa sababu ya mchezo huo kurudishwa nyuma ili kupisha mchezo wa Klabu Bingwa Afrika ambapo Simba atamkaribisha As Vita kutoka nchini Congo,wameikubali sababu hiyo na mchezo wao utachezwa kesho saa 1.00 usiku katika Uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex uliopo Chamazi.
.
“Awali mchezo wetu ulipangwa kuchezwa jumamosi lakini baada ya Bodi ya Ligi kutuambia mchezo huo utachezwa kesho kwa sababu siku na muda wa mechi yetu ni sawa na ratiba ya mechi ya Simba,swala hilo tumelipokea na mchezo wetu utachezwa kesho kwa kuheshimu ukubwa wa mechi itakayochezwa siku ya jumamosi” amesema Maganga