Klay Thompson avunja rekodi ya Steph Curry
Steph Curry akiwa anashikilia rekodi yake ya NBA ya kufunga pointI 3 13 katika mechi moja aliyojiwekea Novemba 2016 kwenye mechi yao dhidi ya Orleans pelicans, mchezaji mwenzake wa Warriors Klay Thompon aliivunja hapo juzi katika mechi yao dhidi ya Chicago Bulls.
Mechi hiyo iliisha kwa Golden State Warriors kuibuka na ushindi wa points 149 – 124 huku Klay Thompson akifunga points 3 mara 14 na kufanikiwa weka rekodi mpya.
Katika mechi ya hiyo dhidi ya Chicago wakati wa mapumziko, Klay alikuwa tayari ashapiga Pointi 3 10, Steph akamwambia Klay kuwa “ Go Get it “ . Akimpa ruhusa ya kwenda kuvunja rekodi yake.
Ni ishara ya kuonesha Steph Curry kutokuwa mbinafsi.
Kipindi cha pili Klay akaenda na kufikisha Pointi 3 14 na hivyo kuvunja rekodi ya Steph
Kwa upande wa Curry ambaye anatajwa kuwa mfungaji bora wa pointi 3 kuwahi kutokea duniani, bado anashikilia rekodi ya mchezaji aliyefunga pointi 3 nyingi katika msimu mmoja akiwa amezifunga mara 402 msimu 2015-16.