KAULI YA TAMBO YA RONALDO BAADA YA KUITOA ATLETICO KISHUJAA
Baada ya kufanikiwa kufunga magoli matatu (hat-trick) katika ushindi wa 3-0 wa Juventus dhidi ya Atletico Madrid na kuipeleka timu yake katika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Cristiano Ronaldo alifanya mahojiano na Sky Sports Italia na kueleza kwa nini Juventus walimua kumsajili yeye.
Ronaldo ambaye amepindua matokeo hayo na kufuzu kwa ushindi wa jumla ya aggregate 3-2, hat-trick ya Ronaldo inakuwa ni hat-trick yake nane katika michuano hiyo, hivyo baada ya hat–tricki hiyo aliyoifunga huku mpenzi wake Georgina akimwaga machozi ya furaha ameeleza sababu za Juventus kumsajili.
“Huu ulitakiwa kuwa usiku maalum na umekuwa hii ndio akili unayohitaji katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, tupo katika njia sahihi na hii ndio sababu ya Juventus kunileta mimi ni kuisaidia katika usiku wa maajabu kama huu, Atletico ni timu ngumu kucheza dhidi yao, mapema sana kuizungumzia fainali inabidi tuzungumze hatua kwa hatua” alisema Cristiano Ronaldi mbele ya Sky Sports Italia.
Cristiano Ronaldo ambaye ana umri wa miaka 34 kwa sasa anaendeleza makali yake akiwa na Juventus baada ya kuondoka Real Madrid ambayo alidumu nayo kwa misimu 9 toka 2009