CAF IMEENDELEA KUWA NA IMANI YA REFA WA KIKE TANZANIA
Kamati ya waamuzi ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limetangaza orodha ya waamuzi wataochezesha michuano ya fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON U-17) zitakazochezwa mapema mwaka huu nchini Tanzania.
Fainali hizo zitakazochezwa kuanzia mwezi April Tanzania ikiwa ndio nchi mwenye zitachezeshwa na jumla ya waamuzi 29 na kati ya hao waamuzi watatu ndio wakike wamepewa nafasi ya kuchezesha michuano hiyo kwa mara ya kwanza na 26 waliosalia wakiwa wanaume.
Katika orodha ya majina 29 majina 15 ni waamuzi akiwemo muamuzi wa Kike wa kitanzania Jonasia Rukyaa huku 14 wakiwa ni waamuzi wasaidizi ambapo wakike katika orodha hiyo ni wawili, hivyo michuano ya mwaka huu zitaonekana sura za kike katika nafasi ya urefa na muamuzi msaidizi, hii sio mara ya kwanza kwa muamuzi Jonasia Rukya kuchezesha michuano mikubwa amewahi kuchezesha pia fainali za mataifa ya Afrika ya wanawake.