YANGA NA SIMBA ZAPIGWA FAINI
Watani wa Jadi Yanga na Simba wapigwa faini kwa makosa waliyoyafanya katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha Februari 16 mwaka huu.
Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa kulikuwa na vitendo vya ajabu katika mchezo huo kitu ambacho kilipelekea kamati ya masaa 72 kukaa na kutoa maamuzi juu ya Vilabu hivyo.
Kwa upande wa Klabu ya Yanga imepigwa faini ya milioni 6 kwa kosa la kuingia Uwanjani kwa mlango usio rasmi pia kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji kukaguliwa wakiwa koridoni.
Klabu ya Simba pia imepigwa faini ya milioni 3 kwa kuingia Uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.