Pep Guardiola kumfuata Cristiano Ronaldo Juventus
Hii inawezekana ikawa habari ya kushitua zaidi kutokana na kuwa haikuwa imeanza na tetesi na uvumi wa muda mrefu kama ambavyo, hutokea baadhi ya habari za usajili wa wachezaji na makocha kutoka klabu moja na kwenda nyingine, kuna mpya imeripotiwa kwa uzito na kituo kimoja cha redio kuwa kocha wa sasa wa Manchester City Pep Guardiola ataihama timu hiyo.
“Hii ni habari ya mwaka Pep Guardiola tayari ameshaongea na Juventus kuhusu kusaini nao mkataba wa miaka minne, Allegri ataondoka katika klabu hiyo (Juventus) na muhispaniola huyo ndio atakuwa kocha mpya” hii ni taarifa iliyonukuliwa kutoka kituo cha radio cha CRC na muandishi Luigi Guelpa
Pep Guardiola ambaye kwa sasa anaiongoza Manchester City kutetea Ubingwa wake wa Ligi Kuu nchini England, akiwa kaisadia timu hiyo hadi sasa kuwa nafasi ya kwanza ikiwa na alama 74 ilizopata katika michezo 30, wakati Liverpool wanafuatia kwa kuwa na alama 70 wakiwa wamecheza michezo 29, kama utakuwa unakumbuka vizuri Guardiola ambaye amekuwa na mafanikio katika soka alijiunga na Manchester City 2016 akitokea FC Bayern Munich ya Ujerumani.
Imani ya uwezekano wa taarifa hizo kuwa za kweli unakuja kutokana na Luigi Guelpa ndio alikuwa mtu wa kwanza kufichua au kuibua tetesi za nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo kuwa yupo mbioni kujiunga na Juventus akitokea Real Madrid habari ambayo ilitimia miezi michache baadae.