Ben Arfa asema kwa nini alimcheka kocha wa Arsenal
Winga wa zamani wa vilabu vya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa na Newcastle United ya nchini England Hatem Ben Arfa ameeleza kwa nini alimcheka kocha wake wa zamani Unai Emery anayeifundisha Arsenal ya nchini England kwa sasa wakati wamchezo wa Europa League wa hatua ya 16 bora.
Hatem Ben Arfa kwa sasa anachezea Rennes ya nchini Ufaransa ambayo inapambana na timu ya kocha wake wa zamani Unai Emery ambaye amewahi kufanya nae kazi kwa miaka miwili (2016-2018), hivyo mchezo kati ya Rennes dhidi ya Arsenal mchezo wa kwanza ulimalizika Arsenal wakipoteza 3-1.
Hivyo Ben Arfa baada ya ushindi huo alionekana kumcheka Unai Emery ikitafsiriwa kama kejeli kwani hakuwa na mahusiano mazuri sana na kocha huyo wakati akiwa PSG kiasi cha kufikia Unai kumkatan jina lake, sasa Arsenal wakiwa nyumbani kwao Emirates mchezo wa marudiano watahitaji ushindi wa 2-0 na kuendelea ili wafuzu.
“Hamasa yangu ni kucheza mechi ngumu na kupata matokeo yatakayo tuweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, hiko ndio kilichopo kichwani kwangu lakini nimemuona Emery Yule Yule ambaye anatikisa kichwa siku zote, nimemuangalia mara chache na kunifanya nicheke kidogo hajabadilika” alisema Hatem Ben Arfa