Fabregas atibua ujio wa Lampard Stanford Bridge
Baada ya kufungwa goli 6 – 1 katika safari yao ya mwisho Stanford Bridge, safari hii hali ilikuwa tofauti kwa Derby County walioonyesha kucheza vizuri na kuleta upinzani dhidi ya Chelsea ila haikuwa siku yao.
Waswahili wanasema mkubwa mkubwa tu, na ndivyo ilivyokuwa katika mchezo huu ambao uliisha kwa ushindi wa goli 3 – 2. Magoli mawili ya kujifunga kwa mabeki Fikayo Tomori aliyepo Derby County kwa mkopo akitokea Chelsea na mwenzake Richard Keogh kipindi cha kwanza yaliiweka Chelsea kifua mbele na mara zote hizi Derby walijitahidi kusawazisha kwa Jack Marriott na Martyn Waghorn kuipati magoli mawili kabla ya mkwaju wa Cecs Fabregas kutua wavuni na kuiandikia Chelsea goli la 3 na kuhitimisha kipigo hiki.
Chelsea sasa watakutana na Bournemouth waliofanikiwa itoa Norwich kwa goli 2 -1 goli la Steve Cook dakika ya 73 likiwapa ushindi Bournemouth.