Chakula chamletea magoli Lukaku
Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa Man United Romelu Lukaku amemaliza ukame wa kufunga magoli mara baada ya kubadilisha aina ya chakula alichokuwa anakula kabla ya mechi.
Awali alikuwa anakula chakula kinachoitwa ‘Pasta’ na sasa anakula ‘ham & Cheese Omellete’ ambacho hutengezwa kwa mayai na siagi au mafuta
Inaelezwa kuwa tangu abadili aina ya chakula upepo wa kufunga magoli umemgeukia ambapo amefunga goli mbili katika kila mechi kwenye mechi tatu za mwisho.