FA yampiga rungu Pochettino
Chama cha soka England FA kimetangaza rasmi kumuadhibu kocha mkuu wa tikmu ya Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino baada ya kubainika na kujiridhisha kuwa alitenda kosa la kugombana na muamuzi Mike Dean.
FA imetangaza kumfungia Mauricio Pochettino mechi mbili kukaa katika benchi na faini ya pauni 10,000 (Milioni 31) kutokana na kosa hilo alilolifanya licha ya kuomba radhi na kukiri kuwa alikosea na kupandwa na jazba kiasi cha kushindwa kujizuia.
Tukukumbushe kocha Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino aligombana na muamuzi Mike Dean baada ya mchezo wa Tottenham dhidi ya Burnley Februari 23 2019, baada ya mchezo huo kumalizika kwa Tottenham kufungwa kwa mabao 2-1.