Kumbe Barca walimtuma De Jong awaue Madrid
Kabla ya mchezo wa jana kati ya Real Madrid na Ajax Santiago Bernabeu, kiungo wa Ajax Frank De Jong alifunguka kuwa na deni na klabu ya Barcelona ambao walimtuma kuhakikisha wanaitoa Real Madrid kwenye hatua ya 16 Bora ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Frank De Jong mwenye umri wa miaka 21 amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia FC Barcelona akitokea Ajax kwa dau la pauni milioni 65 lakini FC Barcelona imemuacha aendelee kuichezea Ajax kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu ndio ataungana na timu.
Frank De Jong alieleza kuwa alivyoenda Nou Camp kusaini mkataba mwezi Januari mwaka huu, aliambiwa na viongozi wa Barcelona ahakikishe anaitoa Real Madrid ambayo kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ya Ulaya.
“Wakati ninasaini mkataba wa kujiunga na FC Barcelona, (viongozi) waliniomba nihakikishe naitoa Real Madrid katika michuano ya Ligi ya Mabingwa pia kuwa hiyo itakuwa nzuri zaidi kwao”.
De Jong hakutaka kuwaangusha waajiri wake wapya, licha ya kupoteza 2-1 kwenye mchezo wa kwanza nchini Uholanzi, jana akishirikiana na wenzake wakafanikiwa kuifunga Real Madrid goli 4-1 Santiago Bernabeu na kufuzu hatua ya robo fainali,na hivyo De Jong kulipa deni lake na Barcelona.