Mikosi yazidi kumuandama Sanchez Man United
Maisha ya Alexis Sanchez yanaendelea kuwa mabaya katika klabu ya Man United tangu atue klabuni hapo akitokea Arsenal Januari 2018.
Sanchez atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne mpaka sita akiuguza maumivu ya goti lake, amethibitisha kocha Ole Gunnar Solskjaer.
Mchezaji huyo alipata maumivu hayo kwenye mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi Southampton ambapo alitolewa katika dakika ya 52.
Imeripotiwa kuwa timu ya madaktari ya Chile wanasema mchezaji huyo anaweza kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili.