Wacongo kuchezesha mechi ya Simba
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limewatangaza waamuzi kutoka nchini DR Congo kusimamia sheria 17 katika mtanange wa JS Saoura dhidi ya Simba utakaochezwa Machi 9 mwaka huu jumamosi, mishale ya saa nne usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Waamuzi hao ni Jean-Jacques Ndala Ngambo atakayepuliza kipyenga kutoka Congo na mshika kibendera namba moja Olivier Safari Kabene nae kutoka Congo wakati mshika kibendera wa pili Soulaimane Amaldine akitokea Comoro.
Simba wameondoka leo jijini Dar es salaam kwenda nchini Algeria kupitia Dubai tayari kwa mchezo huo.