Mimba haijamzuia dada huyu kusakata kabumbu
Sydney Leroux ambaye ni mshambuliaji wa Orlando Pride ya ligi ya soka ya wanawake ya Marekani, ame-trend mitandaoni kwa kuanza mazoezi ya Pre-Season na timu yake huku akiwa na ujauzito wa miezi mitano na nusu.
Msimu mpya wa ligi unataraji kuanza mwezi ujao.

Mmarekani huyo,28, ameolewa na mshambuliaji Dom Dwyer wa Orlando City ya ligi ya soka ya wanaume ya Marekani, na tayari wana mtoto mmoja wa kiume