Jose Mourinho kutoa hatma ya kutafuta Mkurugenzi wa ufundi
Man United imefanya mazungumzo ya kumuajiri mkurugenzi wa ufundi wakiwa na lengo kuja kufanya kazi ya kuleta wachezaji wapya, lakini maamuzi hayo hayatafanyika mpaka kocha Jose Mourinho apitishe suala hilo.
Kituo cha ESPN kimeripotiwa kuwa, Man United wamefanya majadiliano hayo kufuatia na kufanya vibaya katika dirisha la usajili lililopita ambapo ilileta mvutano baina ya Mourinho na makamu mwenyekiti mtendaji Ed Woordward.
Woodward na bodi ya Man United wameweka nia ya kufufua njia ya klabu ya kuleta wachezaji wapya na wanaamini kuwa chaguzi ya kuleta mkurugenzi wa ufundi itasaidia sana.
Mourinho ametimua kiasi cha zaidi ya pauni milioni 360 katika kuleta wachezaji tangu atue Old Trafford mwaka 2016 , lakini katika dirisha la usajili lililopita aliachwa mwenye hasira baada kupewa pauni milioni 68 tu kwa ajili ya kusajili.