Redknapp awapa makavu Spurs
Kocha wa zamani wa timu ya Tottenham Hotspurs ya nchini England Harry Redknapp amegonga tena vichwa vya habari baada ya kutoa mtazamo wake kuhusiana na Tottenham Hotspur ya sasa na kukiri kuwa bado kwake hajaona chochote kipya katika timu hiyo.
Redknapp ambaye ana umri wa miaka 72 kwa sasa aliwahi kuifundisha timu ya Tottenham Hotspurs kwa kipindi cha miaka minne toka pale alipojiunga nayo kama kocha mkuu 2008 akitokea Portsmouth na kuachana na timu hiyo 2012 na kujiunga na Queen Park Rangers aliko dumu kwa miaka mitatu
“Kiukweli kabisa ninafikiria Tottenham Hotspur walikuwa wazuri zaidi miaka miwili iliyopita, sio sasa, wakati Kyle Walker alikuwa anacheza beki wa kulia katika timu hiyo na alikuwa katika kiwango na Dembele nae alikuwa juu” alisema Harry Redknapp akihojiwa na ITV Sport ya England.
Msimu huu unaanza hadi unaisha Tottenham haijafanya usajili wa mchezaji mpya yoyote katika madirisha yote mawili na wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini England wakitofautiana kwa alama 10 dhidi ya Manchester City wanaoongoza Ligi na alama 9 dhidi ya Liverpool waliopo nafasi ya pili, Kyle Walker kwa sasa yupo Manchester City na Dembele kaenda China.