Man U hakuna cha afadhali
Timu ya Manchester United inakumbana na wakati mgumu katika mchezo wake wa marudiano wa klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya klabu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa, Manchester United wanakabiliana na mitihani miwili katika mchezo huo.
Mtihani wa kwanza wanaokabiliana nao Manchester United katika mchezo huo ni mtihani wa kuhitaji kupindua matokeo ya mchezo huo siku ya Jumatano katika jiji la Paris, baada ya mchezo wa kwanza Old Trafford kupoteza kwa magoli 2-0, hivyo ili waingie robo fainali watahitaji ushindi wa magoli 3-0 na kuendelea.
Pamoja na hiyo kuonekana inaweza kuwa mtihani kwao wakati huu PSG wakiwa wanawakosa nyota wao kama Neymar na Edinson Cavani wanaouguza majeraha, Manchester United katika mchezo huo itawakosa jumla ya wachezaji wake 10 kwa sababu mbalimbali Paul Pogba (adhabu), Sanchez, Herrera, Lingard, Mata, Matic, Phil Jones, Martial, Matteo Darmian na Valencia ambao ni majeruhi.