Yanga kuingia kambini kuwawinda KMC
Kikosi cha Yanga SC kinatarajia kuingia Kambini kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya KMC.
Mchezo huo ambao Yanga ndio mwenyeji utachezwa Machi 10 mwaka huu saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha mkuu wa Klabu hiyo Mwinyi Zahera amesema kuwa kabla ya mchezo wao wa Jumapili atakuwa amefanyia marekebisho safu yake ya ulinzi maana aliyaona mapungufu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Alliance FC ya mwanza japo walishinda.
.
“Kuna makosa niliyaona katika mchezo wetu uliopita tuliocheza na Alliance FC ila kabla ya mchezo wetu wa jumapili nitayarekebisha makosa hayo na tutafanya vizuri katika mechi hii.amesema Zahera.