Nyota wa England alivyonusurika kwenye Madawa ya kulevya
Nyota wa Watford Troy Deeney ameamua kueleza ukweli wa maisha yake aliyowahi kupitia kipindi alipozaliwa na kukulia katika mji wa Birmingham nchini England.
Deeney ambaye enzi za utoto wake baba yake alitumia muda mwingi kuwa jela, alikulia katika mazingira magumu na alishawekwa nyuma ya nondo mara nyingi kutokana na matukio ya mtaani.
Ameweka wazi kuwa mtazamo wake ulikuwa hasi kuhusiana na wachezaji mpira, Deeney aliwahi kukamatwa katika kesi mbalimbali sana za kusababisha vurugu ila kwa sasa amekuwa na kubadilika kiasi cha kufikia kuanzisha taasisi yake ya kusaidia watoto wenye uhitaji maalum.
Deeney mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa akiiongoza safu ya ushambuliaji ya Watford wakati anafanya mahojiano na BBC 5 Live alipoulizwa kuwa alikotoka aliwahi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya au kutumia? .
“Sijui kama unajua historia yangu nilipotokea? Sikukulia katika familia ya daraja la kati ambayo kila mmoja angeweza kuwa katokea huko.
Wauza madawa (Birmingham) walikuwa wanamiliki magari mazuri, wana vifaa vizuri vya mazoezi , nguo nzuri na wachezaji wote waliokuwa wanatokea eneo hilo walifanya hayo yote na kuondoka kwenye eneo hilo.
Niliwahi kutamani kuwa hivyo lakini sikuwahi kugusa madawa katika maisha yangu” alisema Deeney .
“Siku zote nilikuwa nikiamini kuwa pesa ndio itakuletea furaha na kutatua kila kitu katika maisha kumbe huo ulikuwa ni uongo mkubwa niliyowahi kuambiwa” alisema Deeney ambaye ni raia wa England ambaye alizaliwa na kukulia katika mazingira magumu sana, hakutoka katika familia ya daraja la kati ametoka familia ambayo ina matatizo pakuishi tu shida.