Adam Salamba sasa yuko sawa
Baada ya kuumia katika mchezo wa jana ulio wakutanisha Stand United na Simba SC Mshambuliaji wa Simba SC Adam Salamba sasa anaendelea vizuri.
Salamba alishindwa kuendelea na mchezo huo na nafasi yake ilichukuliwa na Medie Kagere dakika ya 45,baada ya kuumia wakati akirukia mpira juu na baada ya kushuka chini akashuka vibaya na kuumia maeneo ya goti la kulia ,ndipo akakimbizwa katika Hospital ya Mkoa Shinyanga.
Akizungumza na #worldsports14 kwa njia ya Simu Salamba amesema kuwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.
“Ninamshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri . Niliumia maeneo ya goti la kulia lakini baada na kupata matibabu sasa nipo sawa na namshukuru pia Mungu kwa ushindi tulio upata dhidi ya Stand United “amesema Salamba
Salamba mpaka sasa ameifungia magoli matano timu yake katika Ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu.