Dalili nyingine za Solskjaer kupewa Man United
Tunapoelekea kuna uwezekano mkubwa kocha wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atakabidhiwa timu hiyo jumla mwisho wa msimu ambapo ndio mkataba wake wa muda utakuwa unamalizika, uvumi wa Ole kupewa nafasi hiyo unazidi kushika kasi mitandaoni ukizingatia Manchester baadhi ya watu wenye nguvu katika soka England kumpigia chapuo.
Achilia mbali kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp kuonesha imani ya moja kwa moja kwa Ole Gunnar Solskjaer akiwa mbele ya waandishi wa habari, ila kuonekana katika baadhi ya miradi ya msimu ujao ya Manchester United kuna ashiria kuwa kocha huyo kuna uwezekano bodi ya wakurugenzi imempitisha ila inasubiri mwisho wa msimu kumtangaza rasmi.
Ole Gunnar Solskjaer sasa ataonekana katika tangazo la Manchester United la msimu ujao la kuhamasisha mashabiki wa Manchester United wanunue tiketi mpya za msimu ujao wa Ligi, kwa kawaida vilabu vya soka Ulaya vinapokuwa vinazindua, miradi au jezi mpya za msimu unaofuatia huwa zinawatumia wachezaji ambao zina uhakika kuwa zitakuwa nao msimu ujao.
Hivyo kuthibitika kuwa Ole ataonekana katika tangazo hilo kuna ongeze alama za matumaini kwa nguli huyo kuwa kawekwa katika mpango wa muda mrefu wa Manchester United hivyo atakabidhiwa timu.
Hadi sasa ukiachilia mbali kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG, Ole Gunnar Solskjaer akiwa kocha wa muda wa Manchester United hajapoteza mchezo hata mmoja wa Ligi Kuu akiongoza katika michezo 12, Ole ameshinda michezo 10 na sare miwili huku michezo sita akicheza pasipo kuruhusu bao.