Sanamu ya Beckham yazinduliwa Marekani
Timu ya LA Galaxy ya nchini Marekani leo imezindua rasmi sanamu ya mchezaji wao wa zamani David Beckham ambaye amekuwa ni mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi ya soka ya Marekani (MLS) kujengewa sanamu.
Sanamu hiyo imejengwa kwenye mlango mkuu wa kuingilia uwanja wa timu hiyo
David Beckham aliichezea LA Galaxy kwa miaka sita, ambapo alijiunga nao mwaka 2007 akitokea Real Madrid.
Timu hiyo imeamua kufanya hivyo ikiwa ni kutoa heshima kwa Muingereza huyo ambaye aliwasaidia kushinda kombe la MLS mwaka 2011 na 2012 na ujio wake katika ligi hiyo uliwavutia mastaa wengine kutoka Ulaya kwenda kucheza, kama vile Thiery Henry, Didier Drogba , David Villa na wengine wengi