Simba vitani kesho dhidi ya Stand
Baada ya Ligi Kuu Tanzania bara kuendelea kwa mchezo minne leo,Kikosi cha Simba kitashuka Dimbani kesho dhidi ya Stand United katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara amesema kuwa mchezo huo ni mchezo muhimu na ni sehemu ya mwisho ya maandalizi ya mchezo wao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya JS Soura utakaochezwa Machi 9 nchini Algeria.
“Mchezo wetu wa kesho dhidi ya Stand United ni mchezo mzuri na mchezo utakuwa mgumu maana Stand sio timu mbaya ila timu itakayocheza vizuri ndio itaondoka na point tatu,mchezo huu kwetu ni mchezo muhimu na ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kabisa kabla ya kuelekea nchini Algeria kuwa kabiri JS Soura hapo machi 9 mwaka huu” amesema Manara
Simba anakutana na Stand United akiwa amecheza michezo 19 ana point 48 na anashika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara, huku Stand United akiwa amecheza michezo 28 point 33 nafasi ya 11.