Arrizabalaga kuendelea kutumikia kifungo
Kocha wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri amesema kipa Arrizabalaga kutocheza mechi ya jana dhidi ya Spurs ilikuwa ni maamuzi sahihi na kusisitiza kuwa Mhispania analipia kosa alilolifanya.
Sarri pia amesema kuwa Kepa ataendelea kuwa chaguo lake la kwanza klabuni hapo , lakini anamkabidhi Willy Caballero majukumu ya kipa katika mechi mbili zifuatazo, dhidi ya Fulham na Dynamo Kiev.
Kipa huyo tayari alishaadhibiwa kwa kukatwa mshahara wake wa wiki moja kwa kosa lake la kukataa kufanyiwa mabadiliko kwenye mechi ya fainali ya kombe la ligi dhidi ya Man City jumapili iliyopita Februari 24