Joe Hart kwenda kula mafao Marekani
Moja kati ya mataifa makubwa ambayo yanapambania kukuza Ligi zao kwa kuleta wachezaji wenye majina ni pamoja na Ligi Kuu ya nchini Marekani (MLS) ambayo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikichukua wachezaji wenye majina na umri mkubwa kutoka Ligi mbalimbali kubwa duniani ili kuongeza mvuto katika ligi hiyo.
Mara nyingi wachezaji wanaokwenda kucheza Ligi ya Marekani kutokana na kwenda wakati wakiwa na umrimkubwa huwa kwa utani Ligi hiyo inaitwa Ligi yawastaafu, hivyo baada ya kuanza kuenea tetesi za mlinda mlango wa zamani wa Manchester City anayecheza Burnley Joe Hart kuhusishwa na kwenda nchini humo.
Habari za uhakika zinadaiwa kuwa mlinda mlango huyoambaye kwa misimu yahivi karibuni amekumbwa na haliya kutolewa kwa mkopo kabla ya kujiunga jumla na Burnley 2018, anataka kwenda kujiunga na klabua namoja kati ya klabu nchini Marekani ambazo hazijawekwa wazi, kwa sasa Joe Hart ana umri wa miaka31 ila amekuwa na wakati mgumu sana katika sokakutokana na kutopata nafasi ya kutulia na timu moja kwamuda mrefu kwani Manchester City imekuwa ikimtoa kwa mkopo.