Arrizabalaga apigwa faini Milioni 500 Chelsea
Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga amepigwa faini ya mshahara wake wa wiki moja ambao ni pauni 190,000 na amewaomba msamaha wachezaji wenzake na klabu hiyo kwa ujumla kwa kosa alilofanya jumapili iliyopita Februari 24 kwenye fainali ya kombe la ligi dhidi ya Man City ambapo alikataa kutoka nje wakati kocha Maurizo Sarri akitaka kumfanyia mabadiliko.
Pesa hiyo aliyopigwa faini ambayo ni sawa na Tsh Milioni 586 zitaenda katika Foundation ya Chelsea.
Kocha Maurizio Sarri alisema kuwa alifanya mazungumzo mazuri na kipa huyo baada ya mchezo na kueleza kuwa hali ile ilitokea kutokana na kutoelewana kwenye mawasiliano.
Sarri ameongeza kuwa Kepa aligundua kuwa amefanya kosa kwa vile alivyofanya na akaomba msamaha kwake, wachezaji wenzake,klabu nzima pamoja na mashabiki wote.