Mbinu aliyotumia Solskjaer kupunguza makali ya Liverpool
Baada ya kukumbwa na balaa la majeruhi kipindi cha kwanza hapo jana, benchi la ufundi la Man United lilitoa maelekezo kwa Ball Boys wote uwanjani kuwa wacheleweshe kuwapa mipira wachezaji wa Liverpool ili kupunguza kasi ya mchezo.

Inaripotiwa kuwa kocha Ole Gunnar Solskjaer ndiye aliyetoa ujumbe huo ambao moja ya staff wa United alianza kuusambaza kwa kila boll boy uwanjani kwenye kipindi cha kwanza wakati tayari wakiwa wamemaliza Substitutions zote tatu.

Mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kwa pande zote, uliisha kwa timu zote kuondoka na pointi moja, matokeo yakiwa sare ya 0-0
