Haruna Moshi amtolea uvivu Jerry Muro
Mkuu wa wilaya ya Arumeru na afisa habari wa zamani wa Yanga Jerry Muro pamoja na kuomba radhi hadharani kupitia ukurasa wake wa instagram kwa Haruna Moshi, Mrisho Ngassa, Kocha Zahera na Yanga kwa ujumla, kutokana na kauli yake aliyoitoa iliyotafsiriwa kuwakosea heshima wachezaji hao na kocha wao, kiungo wa timu hiyo Haruna Moshi Boban ambaye ni moja kati ya waliokosewa, ameyatoa ya moyoni kuhusu kauli ya Muro baada ya kumalizika kwa mchezo wa ASFC mjini Lindi dhidi ya Namungo FC iliyomalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa 1-0 pongezi za dhati kwa mpachikaji bao hilo Heritier Makambo.
Awali Jerry Muro akihojiwa alieleza kuwa Yanga inasajili wachezaji wa aina gani wale huku akitolea mfano kuwa Mrisho Ngassa kuwa kwa sasa anatakiwa atafute kazi nyingine ya kufanya huku akisema Haruna Moshi Boban ndio amekwisha kabisa
.
“Watu wa aina gani unawaingiza Ngassa amecheza timu hii miaka na miaka simchukii Ngassa ni rafiki yangu lakini Ngassa nae aangalie kazi nyingine ya kufanya akajifunze ukocha awe hata kocha wa vijana sio lazima ang’ang’anie kucheza mpira haya sasa Boban nae yuko pale anatafuta nini yule mwili umechoka maisha yake yamechoka akili yake imechoka”alinukuliwa Jerry Muro katika sauti iliyokuwa inasambaa mitandaoni
Hata hivyo Boban nae ameamua kutoka kukaa kimya licha ya mwenzake Mrisho Ngassa kuamua kupotezea na kutokana kusema chochote zaidi ya kukiri mkubwa hakosei kazi yake ni kucheza mpira tu.
.
“Kweli amenidhalilisha mimi pamoja na familia yangu pamoja na klabu yangu, sisi wanamichezo tunakosea kuwaweka watu ambao sio wanamichezo, inabidi wanamichezo tuliangalie hilo, haya ndio yanayoleta matatizo na kushindwa kuendelea kwa mpira wetu, unapoongea shirikisha kwanza Ubongo wako” alisema Haruna Moshi Boban baada ya mchezo