Sarri kawashangaa wanaoiponda Chelsea na kuipongeza Arsenal
Ushindi wa 3-0 dhidi ya Malmo juzi Alhamisi ni wazi uliipa Chelsea tiketi ya kuingia hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa Ligi moja kwa moja kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-1 , lakini kocha wao mkuu ameoneshwa kukasirishwa na wanaoisakama timu yake wakisema ipo katika hali mbaya na haina na matokeo mazuri.
Maurizio Sarri baada ya kuona maneno yanazidi kuwa mengi na anakosolewa, amehoji kuwa haoni kama wanastahili kukosolewa kwa kiwango hicho, kwani anaamini kuwa hayupo katika nafasi mbaya zaidi ya Arsenal ambao wamekuwa hawakosolewi sana ukilinganisha na wao.
.
“Nimekuwa nikisikia watu wakiipongeza Arsenal kwa kufanya vizuri msimu huu lakini hawajafika hatua ya fainali ya EFL CUP, wana alama sawa na sisi katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchini England, wamefika hatua ya 16 bora Europa League kama sisi tulivyofika, sielewi kwa nini watu wanaufanya kama msimu huu tumefanya vibaya sana na Arsenal ndio wamefanya vizuri” kocha wa Chelsea Maurizio Sarri akiongea na waandishi wa habari
Hata hivyo Maurizio Sarri ambaye anahusishwa kuwa katika wakati mgumu kiasi cha kuanza kuhusishwa ajira yake kuja kurithiwa na kocha Zinedine Zidane, bado ana-pressure ya siku ya Jumapili akicheza mchezo wa fainali ya Kombe la EFL dhidi ya Manchester City, pamoja na hayo Chelsea imepangwa kucheza dhidi ya Dynamo Kyiv hatua ya 16 bora ya Europa League msimu huu.