Klopp ampigia debe Solskjaer OT
Akiwa amefanikiwa kuifundisha Manchester United kwa kipindi kifupi tu toka ajiunge nayo kama kocha wa muda hadi mwisho wa msimu, Ole Gunnar Solskjaer ameanza kutajwa kama kocha mpya wa kudumu wa timu hiyo ambayo ilidumu kwa muda mrefu na Sir Alex Ferguson licha ya David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho kuchemka.
Ole Gunnar ambaye amesifiwa pia na mkongwe wa zamani wa timu hiyo Eric Cantona kwa kufanya mabadiliko na kujenga nidhamu ya soka ya wachezaji wake, pia amepongezwa na kupigiwa chapuo na mpinzani wake ambaye ni kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ambaye anaamini kuwa Solskjaer kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa muda mfupi anaamini mwakani ataendelea pia kuwa kocha wa Manchester United.
.
“Hakuna wasiwasi na ubora wake (Ole Gunnar Solskjaer) na anastahili kupewa kazi jumla (Manchester United) kwa asilimia 100 kwa sasa ndio kocha na hakuna mashaka ataendelea kuwa kocha (Manchester United) mwaka ujao tena hilo liko wazi kutokana na kuwa ameibadilisha timu na kuifanya kama ilivyokuwa kwa Ferguson” alisema Jurgen Klopp kuelekea mchezo wao

Liverpool itacheza dhidi ya Manchester United ya Ole Gunnar Solskjaer kwa mara ya kwanza Jumapili hii ya Februari 24 2019 toka amewasili kocha huyo Old Trafford, mchezo wa Ligi kuu nchini England utakaochezwa katika uwanja wa Old Trafford, Ole anaingia katika mchezo huo akiwa ameiongoza Manchester United katika michezo 13 na imeshinda 11, sare mchezo mmoja na imepigwa na PSG mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.p