Mnyama aanza safari ya kuwawinda Wanapaluhengo
Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Azam FC na kuibuka na ushindi wa goli 3-1 kikosi cha Simba SC kimeanza safari ya kuelekea mkoni Iringa kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa februari 26 mwaka huu (juma nne)
Meneja wa Klabu hiyo Patrick Rweyemamu amesema kuwa kikosi kinaondoka leo jijini Dar es Salaam na kufanya mazoezi leo mkoani morogoro na kesho kuanza safari ya kuekekea Iringa.
Patrick pia aelezea hali ya sasa ya Emmanuel Okwi ambaye jana alitolewa Uwanjani kwa machela baada ya kuumia, amesema mchezaji huyo anaendelea vizuri na alishonwa nyuzi mbili tatu chini ya jicho ambapo aliumia na yupo katika msafara huo wa kwenda Iringa.