Barcelona yamfukuza kazi mama wa nyota wa PSG
Moja kati ya habari inayotembea katika mitandao ya kijamii ni pamoja na tetesi za nyota wa Paris Saint Germain Adrien Rabiot kutangazwa kuwa ameamua kumfukuza kazi mama yake mzazi kutokana na dili lake la kutaka kwenda kucheza timu ya FC Barcelona ya nchini Hispania kushindikana
.
Baadhi ya mitandao imeripoti taarifa hizo japokuwa Adrien Rabiot mwenyewe hajathibitisha ila taarifa za ndani zinaeleza kuwa kiungo huyo Mfaransa amefikia maamuzi hayo.
Kama hufahamu nyota huyo,23, katika soka wakala wake ni mama yake mzazi lakini baada ya kushindwa kuhakikisha usajili wa kwenda Barcelona kukamilika ameamua kumuweka pembeni na kuanza kuandaa wakala mpya atakayemsimamia.
Adrien Rabiot amekuwa akihusishwa kuwa mbioni kujiunga na timu ya FC Barcelona kwa miezi kadhaa na mpango huo ulikuwa unatarajiwa kukamilika dirisha dogo la Januari, hata hivyo kusajiliwa kwa Frenkie de Jong anayecheza nafasi moja na Adrien Rabiot kumeweka uwezekano mdogo sana kwa FC Barcelona kumuhitaji katika dirisha lijalo la usajili kwani wanacheza nafasi moja.