Mbappe ni mgumu kuliko Messi
Mlinzi wa kati wa kibrazil anayeitumikia timu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa Marcelo Antonio ameweka wazi mawazo yake kuwa kwake imekuwa rahisi zaidi kucheza dhidi ya Lionel Messi kuliko kucheza dhidi ya nyota wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga PSG Kylian Mbappe.
Marcelo Antonio ametoa kauli hiyo baada ya kuwa amebahatika kucheza dhidi ya nyota hao kwa nyakati tofauti tofauti na amebaini kwake kuwa Mbappe ndio alimsumbua walipocheza dhidi yao na kuwafunga katika Ligue 1 kwa mabao 2-1 na kuwa timu pekee iliyofanikiwa kuifunga PSG msimu huu katika Ligi Kuu.
FC Barcelona na Lyon walikutana siku ya Jumanne katika mchezo wa 16 bora wa ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/2019 wakiwa nchini Ufaransa na kujikuta mchezo ukimalizika 0-0, huku hiyo ikiwa ni fursa kwa Marcelo kucheza dhidi ya Messi na kupima uwezo wake kabla ya kurudiana nao Machi 13 2019 Camp Nou.
.
“ Nimecheza dhidi ya Mbappe msimu huu ilikuwa kazi ngumu kumkaba, Messi hakucheza vizuri (SIku ya Jumanne) lakini Mbappe kwa kasi yake, namna anavyojiweka katika nafasi na kucheza na beki ilikuwa ni ngumu kumkaba nafikiri kuna nafasi kubwa siku za usoni akawa mchezaji bora duniani” alisema Marcelo Antonio