Sarri awajibu waandishi kuhusu Kante
Wakati kukiwa na tetesi kuhusiana na kibarua chake ndani ya Stamford Bridge kukaribia kuota nyasi, kocha wa Chelsea Maurizio Sarri mbele ya waandishi wa habari amekubali kulitolea ufafanuzi suala la kutokumchezesha kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeitumikia klabu hiyo N’golo Kante katika eneo lake la asili.
Maurizio Sarri toka amewasili Chelsea Julai 2018 amekuwa mara kwa mara akipenda kumtumia N’golo Kante nje ya eneo lake la asili (holding midfielder) kwa sababu za kudai kuwa mzito kama ambavyo alikuwa akitumika katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi na Chelsea kabla ya ujio wa Sarri.
.
“Wengi wanalaumu kuwa unakaidi kumchezesha N’golo Kante nafasi ambayo alikuwa anacheza akiitumikia Ufaransa na Chelsea hapo awali?” –Ripota
“Inategemea namna mpira unavyouona na hiyo nafasi unayoitaka acheze anatakiwa kuuamisha mpira kwa haraka sana ila hiyo sio moja kati ya sifa za N’golo, N’golo ana manufaa kwetu, lakini hii si moja ya sifa yake “ -Maurizio Sarri
.
“Akicheza nafasi yake ya awali amefanikiwa kushinda Kombe la Dunia na mataji mawili ya Ligi Kuu England?”-Mwandishi
.
“Lakini hiyo ni kwa mfumo mwingine sio huu”-Maurizio Sarri
Kwa sasa kukiwa na uvumi mzito wa Maurizio Sarri kutaka kufutwa kazi katika kikosi hicho kutokana na mwenendo wa timu kutouridhisha uongozi, makocha wawili pekee ndio wamekuwa wakihusishwa kurithi kiti hicho ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo Frank Lampard na kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane.