Jerry Murro awaomba radhi Yanga
Mkuu wa wilaya ya Arumeru na afisa habari wa zamani wa Yanga Jerry Muro kutokana na kauli nzito na kudaiwa za kuwavunjia heshima wachezaji wa Yanga na kocha wao, ameamua kuomba radhi hadharani kupitia ukurasa wak wa instagram, hiyo ikiwa ni siku moja imepita toka aitamke kauli hiyo.
“Niwaombe Radhi,wanachama, mashabiki wote wa @yangasc waliokerwa na kauli yangu dhidi ya mwalimu zahera na Ngasa na Boban, Tukumbuke na mimi naumia tunapoona timu Kubwa ya kimataifa kama yanga inashindwa kufanya vizuri dhidi ya simba INAUMA, lakini maneno yangu yabaki changamoto Kwa Ngasa na Boban kufanya vizuri ili kudhihirisha niliyayotoa Kwa makosa , tunaendelea kujifunza Kutokana na makosa #YangaDaimaMbele” aliandika Jerry Muro kupitia ukurasa wake wa instagram
Awali Jerry Muro akihojiwa alieleza kuwa Yanga inasajili wachezaji wa aina gani wale huku akitolea mfano kuwa Mrisho Ngassa kuwa kwa sasa anatakiwa atafute kazi nyingine ya kufanya huku akisema Haruna Moshi Boban ndio amekwisha kabisa
“Watu wa aina gani unawaingiza Ngassa amecheza timu hii miaka na miaka simchukii Ngassa ni rafiki yangu lakini Ngassa nae aangalie kazi nyingine ya kufanya akajifunze ukocha awe hata kocha wa vijana sio lazima ang’ang’anie kucheza mpira haya sasa Boban nae yuko pale anatafuta nini yule mwili umechoka maisha yake yamechoka akili yake imechoka”alinukuliwa Jerry Muro katika sauti iliyokuwa inasambaa mitandaoni
Hata hivyo pamoja na Yanga kupitia wakati mgumu kiuchumi na kukosa baadhi ya viongozi wa kudumu wa klabu hiyo, bado wameendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania bara japo sio kwa asilimia 100, Yanga kwa sasa ndio timu inayoongoza Ligi kwa kuwa na alama 61 ikicheza michezo 25 huku ikifuatiwa na Azam FC waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na alama 50 wakicheza michezo 24.