Simba kutua Dar leo, tayari kwa vita dhidi ya Azam
Baada ya ushindi wa jana dhidi ya African Lyon ambapo Simba aliibuka na ushinda wa goli 3-0 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Jijini Arusha kikosi cha Mabingwa hao kimeanza safari ya kurejea jijini Dar Es Salaam kwaajili ya mchezo ujao dhidi ya Azam FC utakaochezwa februari 22 mwaka huu (ijumaa) katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Azam FC anakutana na Simba akiwa amecheza michezo 24 na anashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu na ana point 50, huku Simba akiwa amecheza michezo 17 na anashika nafasi ya tatu na ana point 42.