Azam fc wawafata wagosi
Kikosi cha Azam FC, kimewasili mkoani Tanga, tayari kuvaana na Coastal Union, kesho jumanne kwenye Uwanja wa Mkwakwani katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara utakao chezwa saa 10.00 jioni.
Azam FC amekuwa na matokeo mabaya katika mechi tatu mfululizo, katoka sare ya 1-1 dhidi ya Alliance ya Mwanza, kaenda Iringa katoka sare ya 1-1 dhidi ya Lipuli na mchezo wa mwisho kabla ya kwenda Tanga alikutana na Tanzania Prisons na kupokea kipigo cha goli 1-0.
Je? Azam FC atafukuzia kupata Ubingwa msimu huu?