Chelsea Vs Man United tena kwenye FA Cup
Man United leo watakuwa kibaruani leo kwenye uwanja wa Stamford Bridge kuwavaa Chelsea katika mchezo wa raundi ya 5 kombe la FA
➡️ Hii ni mechi ya 14 ya FA Cup kati ya Chelsea na Man United – The Blues wameshinda katika mechi zote 4 za mwisho walizokutana, ikiwemo kwenye fainali msimu uliopita.
➡️Man United wamepoteza mechi 3 kati ya 5 za FA Cup dhidi ya Chelsea Stamford Bridge, walishinda 5-3 msimu wa 1997/98 na 2-0 msimu wa 1998/99.
➡️ Chelsea wanaweza kuwa ni timu ya kwanza kuiondoa Man United mara 5 mfululizo walizokutana kwenye FA Cup.
➡️ Katika michuano yote, Man United wameshinda mara mbili tu kati ya mechi zao 22 za mwisho za ugenini dhidi ya Chelsea ( D7,L13) , wameshindwa kushinda yoyote kati ya tisa zilizopita.
➡️Man United wamewatoa mabingwa watetezi wa FA Cup mara 10, zaidi ya timu yoyote ile kwenye historia ya michuano. Mara ya mwisho walifanya hivyo 2011/12 dhidi ya Man City.