Borussia Dortmund na Hethra Berlin kuchunguzwa
Borussia Dortmund na Hethra Berlin kuchunguzwa na chama cha soka ujerumani baada ya vurugu za mashabiki
Chama cha soka cha Ujerumani (DFB) kimefungua uchunguzi juu ya matukio yakiyotokea katika mechi ya Dortmund dhidi ya Hethra iliyoisha kwa sare ya 2 – 2 jijini Dortmund siku ya Jumapili.
Polisi wa Dortmund walitoa tamko kuwa watu 45 walijeruhiwa kutokana na vurugu zilizotokea.
Hertha wamelaani vitendo hivyo na chma huru cha mashabiki kimetuhumu polisi kwa operesheni nyingi ambazo hazikuwa na ulazima.
Kwenye tamko la DFB hapo Jumatatu walisema wamefungua uchunguzi dhidi ya matukio hayo na klabu zote mbili zitahitaji toa maelezo.
“Baada ya kupitia maelezo yote na vyanzo vingine ikiwemo Tv na video pamoja na maelezo ya usalama DFB itatoa hatma ya suala hili.” lilisema tamko hilo la DFB
Vurugu zilitokea Westfalenstadion dakika za mwanzo mechi ilipoanza baada ya polisi kujaribu wanyaganya mashabiki wa Hertha bango linalotumika kama moja ya kuadhimisha sikukuu ya Hertha Utra Group Hauptstadtmafia or Capital Mafia. Mashabiki hawa walitumia bango hili kama kizuizi dhidi ya camera na kuanza tumia vilipuzi na baruti hivyo polisi kusema walikuwa wanakamata bango hilo ili kuepusha vurugu zaidi.
Katika viwanja vya Ujerumai matumizi ya vilipuzi na fataki ni kosa ila polisi wamekuwa hawaingilii suala hili miaka ya hivi karibui na badala yake wamekuwa wakitumia teknolojia ya video kuwatambua watumiaji.
Jumamosi mashabiki wa Hertha waliruka juu ya bango hilo hadi karibia na eneo la uwanja kuzuia bango lao kuchukuliwa na polisi na kuwashambulia polisi kwa fimbo za vibendera na toka kwenye video moja mtandaoni imeoyesha kilipuzi kikirushwa kwa polisi na mashabiki.
Muda wa mapumziko vurugu zaidi zilitokea mashabiki wa Hertha walipowashambuia tena polisi kwa mabaki ya chakula katika duru mbalimbali zimeeleza kuwa zaidi ya mashabiki 10 wa Hertha walibakia katika Hosiptali za Dortmund wakipatiwa matibabu.
Katika tamko lao Jumamosi Klabu ya Hertha iliwatuhumu mashabiki wake na kusema watafanya kila liwezekanalo kuwatambua wote waliohusika. Pia walisema wataangaza sababu za doria nyingi za polisi.
Kwa pamoja vyama vya mashabiki wa Hertha na Dortmund wamepinga maamuzi ya polisi kutumia pilipili za kupuliza kutokana na kuwapo kwa kudi kubwa la mashabiki hivyo inaweza zua taharuki na kusababisha tatizo zaidi.
Dortmund iliyokuwa imetoka shida 4 – 0 dhidi ya Atletico Madrid na kuwafanya kuwa na ushindi wa sita mfululizo, walipoteza point siku hiyo baada ya mchezo wao na Hertha kumalizika kwa goli 2 – 2. Mchezaji Sncho aliyeko katika kiwango bora msimu huu ndie aliyeifungia Dortmund magoli mawili huku makosa ya Dan-Axel Zagadou dakika za mwisho yaliiokoa Hertha baada ya kuwasababisha penati iliyoamua matokeo ya sare.