Kinda wa Man United afanikiwa kupambana na kansa
Beki wa kati wa Manchester United Max Taylor ambaye jina lake halali kabisa Max Dunne, ameripotiwa kuendelea vyema na mapambano yake dhidi ya ugonjwa wa kansa ambayo baada ya kufanyiwa upasuaji ataweza kurudi tena na kuendelea na kazi kama kawaida ya kuitumikia Manchester United.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 lakini anacheza katika kikosi cha Manchester United cha U-23, mwaka jana kwa mara ya kwanza aliweza kusaini mkataba wake wa kulipwa
Kwa sasa anaendelea vizuri na matatizo yake ya kansa na ataendelea kufuatiliwa zaidi baada ya kupatiwa matibabu ya awali hiyo ni kwa mujibu wa viongozi wakuu wa Manchester United.
“Naomba nitoe shukrani zangu kwa kila mmoja ndani ya klabu ambaye alikuwa akiniombea toka siku ya kwanza, maneno hayawezi kutosha kuelezea ni kwa kiasi gani familia yangu imenisaidia kuyapita haya mapito, mama yangu, baba yangu wa kambo Matthew, kaka na mpenzi wangu Lydia na wote wanafamilia ambao wamekuwa wakitoa sapoti isioweza kuelezeka” alisema Max Taylor