Kagere awajibu wanaomuita mzee
Moja kati ya wachezaji nyota wanaotajwa kuunda vyema safu ya ushambuliaji ya Simba ni pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda anayekipiga Simba Meddie Kagere, pamoja na kuwepo na maneno mingi ya kubezwa kwa mchezaji huyo wakidai kuwa ni mzee kwa umri licha ya kufanya vizuri.
Jana Kagere baada ya mchezo wa watani wa jadi alifanikiwa kufanyiwa mahojiano na Azam TV na kuulizwa analipokeaje suala la yeye kuitwa mzee akiwa anacheza Simba, vipi anaipokeleaji maana hiyo ndio imekuwa fimbo kubwa ya kumchapia Kagere kwa upande wa mashabiki wa wapinzani wake.
“Kwangu mimi akili ni muhimu kuliko umri “ alisema Kagere.
“ Kwetu sisi kitu muhimu ni alama tatu hatujali tutakuwa tumefunga magoli mangapi, unaweza kufunga hata magoli 10 au 11 lakini hiko sio kitu muhimu kitu muhimu unafunga moja na upata alama tatu, kwa sasa hii ni historia tunalenga katika mchezo ujao” alisema Meddie Kagere
Ndani ya wiki moja Meddie Kagere ndio amekuwa mkombozi wa Simba katika michezo muhimu ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kwani alifunga goli 1-0 lililowapa alama tatu na kuwaweka nafasi ya pili katika Kundi D, jana Februari 16 pia ameifungia timu yake ya Simba bao katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga mchezo wa Ligi Kuu uliyowafanya wafikishe jumla ya alama 39 wakiwa nafasi ya tatu lakini wana viporo michezo nane tayari wakiwa wamecheza mechi 16 wakati wenzao Yanga mechi 24 na wanaongoza Ligi kwa kuwa na alama 58.