JUVENTUS WAPO TAYARI KUMTOA BURE DYBALA NA PESA WAMPATE MO SALAH
Uongozi wa klabu ya Juventus ya nchini Italia unaonekana umeamua kuendelea kuingia katika historia za kufanya usajili mkubwa na kushitua kila mwaka, kwa leo zimeripotiwa tetesi mpya kuwa klabu hiyo tayari imeonesha dhamira ya dhati ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji wa kimataifa wa Misri anayeichezea Liverpool ya nchini Uingereza.
Juventus wameripotiwa kuwa wapo radhi mwisho wa msimu kumsajili Mohamed Salah kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 44 na kumtoa bure Paulo Dybala kwenda Liverpool kama sehemu ya kuishawishi Liverpool ikubaliane na dau hilo, hivyo ikiwa ni miezi kadhaa imepita toka waingie katika rekodi za kumng’oa Cristiano Ronaldo ndani ya Real Madrid kwa pauni milioni 100.
Inatajwa kuwa kimsingi ogfa hiyo ya Juventus kwa Liverpool haitazamiwi kukataliwa kutokana na klabu hiyo itakuwa imetengeza karibia au zaidi ya pauni milioni 100 kwa kukubali dau hilo na ukijumlisha na thamani ya Paulo Dybala ambayo inatajwa kuwa itafikia pauni milioni 50 na kuendelea kama wataamua kumuuza, hadi sasa Mohamed Salah ndio anaongoza kwa magoli katika Ligi Kuu Uingereza akiwa amefunga magoli 17 sawa na Aguero wa Man City lakini Salah akiongoza kutoa pasi nyingi (7) za usaidizi wa magoli.