MWINYI ZAHERA KAWAITA MASHABIKI WA YANGA“TWENDENI MKAIONE YANGA NYINGINE”
Leo ndio leo msemae kesho muongo, hii ndio siku mashabiki wa soka Tanzania watapata fursa pekee ya kushuhudia Dar es Salaam Derby kwa kushuhudia timu za Simba na Yanga zikicheza mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania bara mzunguuko wa pili msimu wa 2018/2019 ndani ya uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kama ilivyo ada kwa baadhi ya mashabiki wa timu hizo kutambiana kwa maneno ya kejeli ya hapa na pale, kocha mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera mwenye uraia wa Congo na Ufaransa, amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo na kuwaahidi kuwa wataishuhudia Yanga nyingine sio walioizoea.
“Sisi ndio vile tumejitaarisha vizuri sana, tuko vizuri wachezaji wangu wote sina mchezaji yoyote mwenye tatizo kesho tunakuja kama zilivyo mechi nyingine tunavyocheza tukiwa na lengo la kushinda, haitakuwa rashisi itakuwa mechi ya nguvu ndio mimi nawaita kesho mashabiki wa Yanga waje wengi sana wataona Yanga nyingine sio ile Yanga tulicheza mechi nne halafu ya tano tukacheza na SImba hii ya kesho nadhani watashangaa” alisema Zahera kuelekea mchezo huo
Yanga na Simba zinazingia katika mchezo huo, Yanga akiwa anaongoza msimamo wa Ligi kwa kuwa na jumla ya alama 58 akicheza jumla ya michezo 23 wakati watani zao wa jadi Simba wao wapo nafasi ya tano kwa kuwa na alama 36 wakicheza michezo 15 na kuzidiwa michezo nane na Yanga kutokana na Simba kuwa na viporo vingi kutokana na kubanwa na ratiba yake ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ikitokea Simba akivuna alama zote 24 katika michezo nane ya viporo atakuwa na alama 60 na atakuwa na tofauti ya alama 2 zaidi na Yanga.