Spurs kumpiga kitanzi Son
Nyota wa Tottenham Son Heung-Min alisaini mkataba mpya katika timu hiyo mwezi Julai mwaka jana, lakini Spurs sasa wanataka kumpa mkataba mpya mwingine kufuatia kiwango chake ambacho amekionesha mpaka sasa msimu huu.
Imeripotiwa kuwa mazungumzo ya dili hilo yatafanyika kwenye majira ya kiangazi mwaka huu ikiwa ni njia ya kuendelea kumshikilia mchezaji huyo kutoka Korea Kusini.
Son kwa sasa anapokea mshahara wa pauni 110,000 ( Tsh Milioni 328) kwa wiki, na katika dili hilo jipya anataraji mshahara wake kupanda kukaribia mshahara wa Dele Alli paini 150,000 (Tsh Milioni 447) kwa wiki.
Son,26, amekuwa na msimu mzuri, tangu mwezi Oktoba amefanikiwa kufunga magoli 16 kwenye michezo 23 ya michuano yote.