Sala aliliwa na mpenzi wake
Mchezaji wa Volleyball mwanadada Mbrazil Luiza Ungerer alikuwa ni mpenzi wake na aliyekuwa mshambuliaji wa Cardiff Emiliano Sala aliyefariki kwa ajali ya ndege mwezi jana.
Katika njia ya kumkumbuka mpenzi wake Luiza,31, katika mkono wake wa kushoto amechora tattoo ya namba ya jezi aliyokuwa anavaa mchezaji huyo akiwa Nantes, namba 9.
Luiza ambaye anacheza katika timu ya Beziers Angels ya nchini Ufaransa ambapo Sala amekuwa akicheza kwa takribani miaka 10, amepost picha katika mtandao wa Instagram akionesha tattoo hiyo ikiandamana na ujumbe ulioandikwa ‘Para siempre Emi ‘ ikitafsiriwa ‘ Milele Emi ‘ .
Luiza akihojiwa na kituo cha habari cha nchini Brazil, alisema kuwa mara ya mwisho kuonana na Sala ilikuwa katika siku ya kuzaliwa ya Muargentina huyo,28,wiki moja kabla ya kupata ajali.