Loris Karius kurudishwa Liverpool
Klabu ya Besiktas ya nchini Turkey imeripotiwa kutaka kumrudisha kipa Loris Karius katika timu yake ya Liverpool kutokana kutoridhishwa na uwezo wake.
Kipa huyo wa Germany aliruhusiwa kuondoka Anfield majira ya kiangazi mwaka huu na kujiunga na timu hiyo ya Turkey kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili.
Ikiwa imepita miezi mitatu tu ,timu hiyo ya Instabul inataka kumrudisha Liverpool na badala yake wamchukue mshambuliaji Divorce Origi.
Pengine hii itakuwa nafasi nzuri kwa Divock Origi ambaye hajacheza hata dakika moja katika kikosi cha Jurgen KloppĀ msimu huu.
Karius,25, aliwazawadia Real Madrid magoli mawili katika fainali ya klabu bingwa Ulaya msimu uliopita na kufanya Liverpool kupoteza mechi hiy kwa goli 3-1. Baada ya hapo Liverpool wakamsajili Mbrazil Allison Becker kuchukua nafasi yake langoni.
Besiktas ambao kwa sasa wapo nafasi ya nne katika ligi kuu nchini Turkey, pointi 3 nyuma ya vinara Instanbul Basaksehir.
Besiktas wanalipa nusu ya mshahara wa Karius.