Mchezaji wa Singida atua Kenya
Mchezaji wa Singida United Athanasi Mdamu ametua kunako klabu ya Kariobangi Sharks ya Kenya kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Klabu hiyo baada ya makubaliano ya Timu zote mbili.
Mkurugenzi mtendaji wa Klabu hiyo Festo Sanga amesema kuwa Athanas amekwenda Kenya baada ya klabu ya Kariobangi Sharks kumuona na kumpenda katika michuano mbalimbali ya hapa nchini.
.
“Viongozi wa Sharks waliwasiliana na Klabu na baadae kumruhusu mchezaji
huyo aende akaongeze maarifa kwenye soka kwa manufaa yake na Taifa letu.
Hii ni mwendelezo wa program ya Singida United kuwaruhusu wachezaji kwenda kucheza soka nje ya nchi pale tu wanapopata timu kama ambavyo mkataba wa timu na mchezaji unavyoeleza,
Huyu ni Athanas amekwenda Kenya, tunategemea mchezaji mwingine kuondoka siku za karibuni kwenda kucheza barani ulaya na taratibu zake zote zimeshakamilika” amesema Sanga