TFF yakubali ombi la Yanga
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeridhia ombi la Yanga la kuahirisha kusikiliza shauri dhidi ya Abdallah Shaibu kwa vile wakati anapata mwito wa kuhudhuria alikuwa mkoani,sasa shauri dhidi yake litasikilizwa katika kikao kijacho, na Kamati haitapokea udhuru wowote isipokuwa kama atakuwa na majukumu katika timu ya Taifa.
Shaibu aliitwa katika kamati hiyo februari 10 mwaka huu baada ya Bodi ya Ligi kupeleka malalamiko dhidi yake lakini Shaibu hakwenda katika kikao hicho kutokana na kuwa na Timu yake ya Yanga nje ya Jiji la Dar es Salaam kwa michezo ya Ligi kuu Tanzania bara.